Rais mstaafu Uhuru Kenyatta asherehekea Krismasi na yatima

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais mstaafu Uhuru Kenyatta siku ya Jumamosi amesherehekea krismasi na makao kadhaa ya watoto nchini .

Miongoni mwa makao ya watoto ambayo Kenyatta alitembelea ni pamoja na Gatundu Children’s Home, Mama Ngina Children’s Home, Mama Fatuma Children’s Home, St Dorcas Educational Centre na Mary Faith Rescue Centre.

Rais huyo wa zamani amekariri haja ya kujumuika na kuwasaidia wasiobahatika katika jamii msimu huu wa sherehe za Krismasi.

Haya yanajiri siku moja baada ya Rais William Ruto kujumuika na maelfu ya wakazi wa Sugoi mjini Eldoret kusherehekea krismasi.

Share This Article