Rais mstaafu Uhuru Kenyatta anahudhuria ibada na hafla ya kuchangisha fedha katika kanisa la Full Gospel katika eneo la Mwingi, kaunti ya Kitui.
Kulingana na picha za moja kwa moja kwenye ukurasa wa Facebook wa kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka, Uhuru ameandamana na viongozi kadhaa akiwemo naibu kiongozi wa chama cha ODM Wycliffe Ambetsa Oparanya, kiongozi wa chama cha DAP-K Eugene Wamalwa, kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka, Gavana wa Machakos Wavinya Ndeti na mwanawe Kalonzo, Kennedy Musyoka.
Kabla ya kuingia kanisani kwa ibada, kiongozi wa zamani wa nchi alipanda mti nje ya kanisa hilo.