Rais Lula wa Brazil amjibu Trump kuhusu ushuru na kesi ya Bolsonaro

BBC
By
BBC
4 Min Read
Andre Borges/EPA/Shutterstock

Rais wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva, ametetea huku iliyomkuta mtangulizi wake Jair Bolsonaro ya kuhukumiwa kifungo cha zaidi ya miaka 27 jela kwa kupanga mapinduzi.

Katika maoni yake yalichochapishwa katika gazeti la New York Times, Lula amekosoa matamshi ya Rais wa Marekani Donald Trump kuwa kesi hiyo ilikuwa ni ya kisiasa na kusema ni “uamuzi wa kihistoria ambao unalinda taasisi zetu na utawala wa sheria katika demokrasia”.

Kiongozi huyo wa Brazil ameandika makala hiyo ili kuanzisha mazungumzo ya wazi na ya kweli na Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye ameweka ushuru wa asilimia 50 kwa bidhaa za Brazil zinazoingia Marekani.

Lula ameliita ongezeko hilo la ushuru “sio tu kwamba ni potofu lakini lisilo na mantiki.”

Mahusiano yamekuwa ya mvutano kati ya Marekani na Brazil katika miezi ya hivi karibuni, tofauti kabisa na uhusiano wa Trump na Jair Bolsonaro alipokuwa rais.

Bolsonaro mara nyingi alionyesha kuvutiwa kwake na Trump, ambaye alimkaribisha katika jumba lake la kifakhari la kifakhari la Mar-a Lago kwa ajili ya mapumziko mwaka 2020.

Lula, kiongozi wa mrengo wa kushoto, anayejulikana kwa kunyoosha, hakumunya maneno yake katika makala yake ya New York Times.

Amesema kuwa katika kipindi cha miaka 15 iliyopita Marekani “imekusanya ziada ya dola bilioni 410 (£302bn) katika biashara na huduma baina ya nchi hizo mbili,” na kusema uamuzi wa kuongeza ushuru unaweza kuwa wa kisiasa tu.

“Serikali ya Marekani inatumia ushuru na vikwazo kuzuia kutoadhibiwa kwa Rais wa zamani Jair Bolsonaro,” Lula aliandika, akimaanisha vikwazo ambavyo Marekani imeviweka kwa jaji wa Mahakama ya Juu ambaye aliongoza kesi dhidi ya Bolsonaro.

Kesi hiyo ilikamilika Alhamisi wakati majaji wanne kati ya watano wa Mahakama ya Juu, walipompata hatia ya mashtaka yote matano aliyokuwa akikabiliwa nayo.

Bolsonaro amehukumiwa kifungo cha miaka 27 na miezi 3 jela – hukumu ambayo mawakili wake wanasema watakata rufaa.

Trump amesema hukumu hiyo “ya kushangaza sana” na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio alitangaza kwamba Marekani “itajibu ipasavyo kuhusu kuhusu hiyio.”

Katika makala yake ya New York Times, Lula alisisitiza kuwa kesi hiyo “si ya kisiasa”.

“Hukumu hiyo ilikuwa matokeo ya kesi kwa mujibu wa Katiba ya Brazili ya 1988, iliyotungwa baada ya miongo miwili ya mapambano dhidi ya udikteta wa kijeshi,” aliandika, akiwakumbusha wasomaji kwamba demokrasia ya Brazili ilirejeshwa mwaka 1985 baada ya miaka 20 ya utawala wa kijeshi.

Lula pia alikanusha shutuma za utawala wa Trump kwamba mfumo wa haki wa Brazil unalenga na kukandamiza makampuni ya teknolojia ya Marekani.

Rais wa Brazil amesema mahakama za nchi yake zilikuwa sahihi kudhibiti intaneti na makampuni ya Marekani hayakutendwa vibaya.

Alihitimisha makala yake kwa kumhutubia Rais Trump moja kwa moja, akimwambia kwamba Brazil bado iko tayari kujadili “chochote ambacho kinaweza kuleta manufaa kwa pande zote”, lakini akamuonya Trump kwamba “demokrasia na uhuru wa Brazil havitajadiliwa.”

BBC
+ posts
Share This Article