Rais Kagame aibuka mshindi katika uchaguzi mkuu

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais wa Rwanda Paul Kagame.

Rais wa Rwanda Paul Kagame ameibuka mshindi katika uchaguzi mkuu ulioandaliwa nchini humo baada ya kupata asilimia 99.15 ya kura zilizopigwa.

Wapinzani wake waligawana asilimia 1 ya kura hizo, ambapo mwanamazingira Frank Habineza na mwandishi wa habari na mwandishi Philippe Mpayimana walizoa asilimia 0.53 na 0.32 za kura mtawalia.

Kagame mwenye umri wa miaka 66 ameiongoza Rwanda tangu mwaka 2000.

Amewashukuru raia wa Rwanda kwa imani yao katika hotuba aliyotoa katika makao makuu ya chama chake cha Rwandan Patriotic Front (RPF).

“Hizi si takwimu tu, hata ikiwa ni 100%, hizi sio nambari tu. Wao wanaonesha kuamini, na hilo ndilo lililo muhimu zaidi,” Kagame alisema.

Hata hivyo, matokeo kamili ya uchaguzi huo yanatarajiwa kufikia Julai 20, 2024 na ya mwisho ifikapo Julai 27.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *