Baraza la kikatiba nchini Msumbiji limetangaza kuwa Rais mteule Daniel Chapo ataapishwa Januari 15, baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi wenye utata wa Oktoba mwaka jana .
Haya yanajiri huku jamii ya kimataifa ikisema kuwa uchaguzi mkuu wa Msumbiji haukuwa huru na wa haki.
Upinzani pia umekuwa ukifanya maandamano tangu kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi ikiripotiwa kuwa takriban watu 290 wamefariki kwa machafuko ya baada ya uchaguzi.
Chapo wa chama tawala cha Frelimo alitangazwa mshindi kwa kupata asilimia 65.17, dhidi ya asilimia 24 za mpinzani wa karibu Venancio Mandlane.
Viongozi wa mataifa ya Kusini mwa Afrika yameomba kusitishwa kwa mapigano huku yakihimiza mazungumzo ili kumaliza mzozo huo wa kisiasa kutoka kwa pande husika.