Rais Assimi Goita wa Mali ajitangaza Waziri wa Ulinzi

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais wa Mali Assimi Goita.

Wiki moja baada ya Waziri wa Ulinzi wa Mali Sadio Camara kuuawa kwenye shambulizi la kigaidi, Rais wa taifa hilo Assimi Goita ametangaza kuchukua wadhifa huo, kupitia kwa televisheni ya serikali.

Kufuatia tangazo hilo, Goita ambaye aliingia madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi, ataongoza moja kwa moja vyombo vya usalama akisaidiwa na Mkuu wa Majeshi ya nchi hiyo, Jenerali Oumar Diarra, aliyeteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Ulinzi.

Camara aliuawa kwenye shambulizi la bomu katika makao yake, huku wanamgambo waliojihami wakitwaa Kaskazini mwa mji wa Kidal kwenye shambulizi kubwa kuwahi kutekelezwa nchini humo katika muda wa miaka 15.

Katika shambulizi hilo, takriban watu 23 waliuawa, Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu watoto UNICEF likiripoti kuwa raia na watoto walikuwa miongoni mwa waliouawa na majeruhi.

Mali imekumbwa na msukosuko wa kiusalama tangu mwaka 2012.

Kundi la wapignaji  linalohusishwa na Al-Qaeda la Jama’at Nusrat al-Islam wal-Muslimin (JNIM), linadhibiti maeneo makubwa katika sehemu za mashinani nchini humu, hususan maeneo ya Kaskazini na Kati.

Share This Article