Kiongozi wa upinzani na chama cha ODM Raila Odinga alipendekeza azikwe ndani ya saa 72 baada ya kufariki kulingana na wosia wake.
Kwa mujibuu wa familia yake, Odinga, aliyefarikiariki dunia jana akiwa na umri wa miaka 80,alipendekeza azikwe kwenye makaburi ya familia yao eneo la Bondo karibu na kaburi la mamake mzazi Mary Ajuma,Ajuma, aliyefariki mwaka 1984.
Maombi ya kitaifa yameratiwa kuandaliwa kesho Ijumaa katika uwanja wa taifa wa Nyayo, kabla ya mwili wake kusafirishwa kwenda Bondo kwa mazishi ya siku ya Jumapili Oktoba 19.