Raila kupeleka kampeni zake za AUC kusini mwa Afrika mwakani

Dismas Otuke
1 Min Read
Raila Odinga akishiriki Mjadala Afrika

Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga anatarajiwa kuendeleza kampeni yake ya kuwania uenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, AUC mapema mwaka ujao katika eneo la kusini mwa Afrika.

Utakuwa mzunguko wake wa mwisho wa kampeni zake baada ya kuzuru Afrika ya kati, magharibi na kaskazini.

Eneo la kusini mwa Afrika lina idadi ya mataifa 16, mengi yakiwa katika jumuiya ya maendeleo ya SADC.

Akihudhuria mdahalo wa Mjadala Afrika uliowashirikisha wawaniji wote watatu Ijumaa iliyopita, Raila aliahidi kuleta mabadiliko kadhaa barani Afrika endapo atachaguliwa ikiwemo kushinikiza uimarishaji wa biashara ndani ya Afrika, kupewa nafasi mbili katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kutafuta suluhu ya Kiafrika kwa mizozo inayokabili bara hili.

Uchaguzi wa AUC utaandaliwa mwezi Februari mwakani huku mshindi akihitaji kupata uungwaji mkono na theluthi mbili ya mataifa 55 ya Afrika.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *