Kiongozi wa upinzani Raila Odinga anatarajiwa kuhutubia kongamano la ugatuzi leo Alhamisi mjini Eldoret, siku moja baada ya kongamano hilo kufunguliwa rasmi na Rais William Ruto.
Raila alikuwa miongoni mwa waanzilishi wa kubuniwa kwa serikali za kaunti, wazo ambalo lilirasimishwa kwenye mabadiliko ya katiba ya Kenya mwaka 2020.
Kongamano hilo litakalokamilika Jumamosi hii na ambalo huandaliwa kila baada ya miaka miwili, huwaleta pamoja viongozi wa matabaka mbalimbali wakiwemo Maseneta na Magavana wa kaunti zote 47 nchini pamoja na wawekezaji.
Raila anatarajiwa kuzungumzia baadhi ya hatua zilizoafikiwa tangu kubuniwa kwa serikali za kaunti mwongo mmoja uliopita.