Mauritius imemuunga mkono Raila Odinga kuwania uenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, AUC katika uchaguzi ulioratibiwa Februari mwakani.
Kisiwa cha Mauritius kilikuwa kimemsimamisha Anil Kumarsingh Gayan kuwania nafasi hiyo dhidi ya Raila, lakini badala yake Gayan akajiondoa kinyang’anyironi .
Kwenye mazungumzo yake kwa njia ya simu baina ya Waziri Mkuu aliyechaguliwa nchini Mauritius Navichandra Ramgoolam, na Rais William Ruto,kiongozi huyo alitangaza kujiondoa kwa taifa lake katika uwaniaji wa nafasi hiyo na badala yake kuunga Kenya mkono.
Kinyang’anyiro cha Uenyekiti wa tume ya muungano wa Afrika sasa kimesalia na Odinga,Waziri wa mashauri ya kigeni wa Djibouti Mahamoud Ali Youssouf na Richard Randriamandrato wa Madagascar.
Atakayechaguliwa mwakani atamrithi Mousa Mahamata Faki wa Chad, ambaye muda wake wa kuhudumu umekamilika.