Raila aunga mkono ugavi wa pesa kwa kuzingatia idadi ya watu

Dismas Otuke
1 Min Read

Kiongozi wa muungano wa Azimio la Umoja Raila Odinga ameunga mkono pendekezo la kutaka ugavi wa pesa kutoka serikali kuu kwa kaunti kwa kuzingatia idadi ya watu.

Raila anasisitiza kuwa hiyo ndiyo mbinu pekee itakayohakikisha kila katunti inanufaika kikamilifu badala ya kuzingatia ukubwa wa kaunti au kupewa kiwango sawa cha pesa za matumizi.

Aliyasema hayo jana Alhamisi alipopokea ripoti ya mkutano wa Limuru 3 katika makao makuu ya chama cha ODM huko Chungwa House.

Raila alisema alikuwa akipendekeza mfumo huo wa ugavi kwenye kamati ya uwiano wa kitaifa maarufu kama BBI.

Mfumo huo umependekezwa na Naibu Rais Rigathi Gachagua kama njia ya kuhakisha kaunti zinapata usawa na haki katika ugavi wa mapato.

Website |  + posts
Share This Article