Raila apongeza serikali kwa kujitolea kuunga mkono azma yake

Kevin Karunjira
1 Min Read

Kiongozi wa upinzani nchini Raila Odinga ameishukuru serikali kwa kujitolea kuunga mkono azma yake ya kuwania uenyekiti wa tume ya umoja wa Afrika, AUC.

Akizungumza na wanahabari leo baada ya kushauriana na waziri aliye na mamlaka makuu Musalia Mudavadi ambaye pia ni waziri wa masuala ya kigeni, Raila alisema amefurahishwa sana na hatua zilizochukuliwa na serikali kumuunga mkono.

Kiongozi huyo alishukuru viongozi wote serikalini ambao wanashughulikia azma yake.

Raila ndiye mwaniaji wa Kenya wa wadhifa huo na sasa serikali imebuni kundi maalamu la kuendesha kampeni yake.

Wakati wa mkutano na wanahabari, Mudavadi alimsifia Raila akisema tajriba aliyo nayo katika uongozi inatosha kuwania kazi hiyo ya Bara Afrika.

Muhula wa miaka minne wa mwenyekiti wa sasa wa tume hiyo ya Umoja wa Afrika AUC Moussa Faki Mahamat, raia wa Chad, unafikia mwisho mwaka ujao wa 2025.

Share This Article