Raila aahidi kupigania Afrika kupewa viti viwili katika baraza la usalama la Umoja wa mataifa

Dismas Otuke
1 Min Read
Raila Odinga akishiriki Mjadala Afrika

Mwaniaji wa Kenya wa Uenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika-AUC, Raila Odinga ameahidi kushinikiza bara Afrika, kupewa nafasi mbili katika Baraza la usalama la Umoja wa mataifa endapo atachaguliwa.

Raila alisema hayo usiku wakai wa mdahalo wa waaniaji watatu wa kiti hicho mjini Adis Ababa ,Ethiopia.

Alisikikitishwa na hali ilivyo kwa sasa ambapo Afrika haina hata kiti kimoja katika baraza la usalama la Umoja wa mataifa, wakati Ulaya  ikiwa na viti vitatu.

Raila pia alielezea ruwaza yake ya kuimarisha na kupika jeki biashara barani Afrika ambayo kwa sasa iko kwa kiwango cha asimilia 15 pekee.

Raila alishiriki mdahalo huo na wapinzani wake wawili,Waziri wa Mambo ya Nje wa Djibouti Mahamoud Ali Youssouf na Richard Randriamandrato, ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani wa Madagascar.

Uchaguzi wa AUC utaandaliwa Februari mwakani huku mshindi akimrithi Mousa  Faki, ambaye amekuwa afisini kwa miaka minne.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *