Raia wawili wa kigeni wakamatwa na pembe za ndovu Mombasa

Tom Mathinji
1 Min Read

Maafisa wa huduma kwa wanyamapori nchini KWS, wamewakamata raia wawili wa kigeni wakiwa na pembe 11 za ndovu.

Paulo Telek na Paulo Kuya wote raia wa Tanzania, walitiwa nguvuni katika mtaa wa Majengo, kufuatia msako wa maafisa hao.

Kulingana na taarifa ya polisi, pembe hizo zenye uzani wa kilo 32.9, zinakadiriwa kuwa za thamani ya shilingi Milioni 3.3.

“Ilibainika kuwa washukiwa hao walisafiri kutoka Tanzania hadi Kenya kutafuta soko la pembe hizo,” ilisema taarifa hiyo ya polisi.

Kwa sasa wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Mtwapa wakisubiri kufikishwa Mahakamani.

TAGGED:
Share This Article