Raia wa Uganda waishtaki kampuni ya TotalEnergies

Tom Mathinji
1 Min Read

Kundi la raia wa Uganda limewasilisha kesi mahakamani dhidi ya kampuni kubwa ya mafuta ya Ufaransa, TotalEnergies mjini Paris, kuhusu miradi miwili mikubwa ya uchimbaji nchini mwao.

Wanadai ukiukaji wa haki za binadamu na wanataka fidia kwa kunyimwa upatikanaji wa ardhi zao.

TotalEnergies inaongoza muungano ambao unachimba mamia ya visima vya uchunguzi na kujenga bomba la mafuta lenye urefu wa kilomita 1,500 ambalo litavuka hifadhi kadhaa za asili nchini Uganda.

Wakati huo huo, polisi wa Uingereza wamewakamata wanaharakati 27 wa mabadiliko ya tabia nchi wanaoandamana kupinga miradi ya Uganda iliyopaka rangi kwenye makao makuu ya TotalEnergies mjini London.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article