Raia sita wa Kenya wameuawa na watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Al-Shabab, katika mpaka wa Kenya na Somalia.
Kulingana na kamanda wa polisi wa kaunti ya Garissa John Samburumo aliyethibitisha kisa hicho, watu hao walikuwa wamevuka mpaka na kuingia nchini Somalia kufungua biashara zao.
Samburumo alisema watu waliokuwa wamejihani kwa bunduki walianza kuwafyatulia risasi kiholela na kuwauwa watu wanne papo hapo huku wengine wawii wakiaga dunia walipkuwa wakipokea matibabu.
Kamishna wa kaunti ya Garissa Mohamed Ramadhan alisema uchunguzi unaendelea kubaini kiini cha kshambulizi hilo.
Aidha aliwataka wafanyabiasha ambao ni raia wa kenya katika sehemu hiyo kuwa makini.