Rachel Ruto: Vijana ni nguzo muhimu katika ustawi wa Kenya

Kevin Karunjira
1 Min Read

Mama wa taifa Rachel Ruto, amesema kuwawezesha vijana ni nguzo muhimu katika kuhakikisha ufanisi wa taifa hili katika siku zijazo. 

Akizungumza leo Jumanne wakati wa mkutano na mwanzilishi wa Jumuiya ya Kimataifa ya Vijana (IYF) Soo Park, nchini Korea Kusini, Mama taifa alisema kuwekeza katika elimu ya vijana, kukuza zao na kuwapa fursa za kujiendeleza, kutahakikisha siku zijazo zilizo na matumaini na maendeleo.

“kuwawezesha vijana, ni nguzo inayohakikisha ufanisi kwa taifa hili katika siku zijazo,” alisema Mama Taifa Rachel Ruto.

Jumuiya ya IYF imejitolea kuwaunganisha vijana na fursa za kubadilisha maisha na inaendesha chuo cha vijana cha wikendi bila malipo kwa ushirikiano na Talanta Hela.

“Huwa navutiwa na mashirika kama vile IYF, ambayo husababisha mabadiliko makubwa katika maisha ya vijana,” alisema Mama Taifa.

Aidha alisema juhudu za IFY zinawiana na ruwaza za taifa hili za kukuza na kuwekeza katika vijana ambao ndio mwanga wa siku zijazo za taifa hili.

Mama taifa ameandamana na Rais William Ruto katika ziara rasmi nchini Korea Kusini.

TAGGED:
Share This Article