Polisi wameawarushia vitoza machozi wafuasi wa waliojitokeza mjini Kakamega siku ya Jumamosi kuhudhuria mkutano wa kisiasa ujulikanao kama Linda Mwananchi, ulioongozwa na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna.
Sifuna alikuwa akiwahutubia wafuasi wake waliofurika katika uwanja wa Amalemba wakati polisi walipofyatua vitoza machozi.
Seneta huyo aliyeandamana na mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino, ameahidi kuandaa mikutano ya kisiasa kote nchini.
Mkutano huo ulikuwa wa pili kwa Sifuna baada ya kuandaa mwingine mjini Kitengela wiki jana siku kadhaa baada ya kutumuliwa katika wadhfa wake wa Katibu Mkuu wa chama cha ODM, kabla ya mahakama kusitisha hatua hiyo.
