Qatar yawahamisha wakazi karibu na Ubalozi wa Marekani mjini Doha

radiotaifa
1 Min Read

Qatar imeanza shughuli ya kuwahamisha wakazi wanaoishi karibu na Ubalozi wa Marekani mjini Doha kama hatua ya tahadhari ya muda, kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Qatar.

“Malazi yanayofaa yametolewa kwao kama sehemu ya hatua muhimu za tahadhari,” Wizara ilisema katika taarifa kwa mtandao wa kijamii wa X.

Hii inakuja baada ya balozi za Marekani nchini Saudi Arabia na Kuwait, na ubalozi mdogo wa Marekani mjini Dubai, kushambuliwa na ndege zisizo na rubani wiki hii.

Mapema wiki hii Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilitoa witio kwa kwa raia wa Marekani kuondoka haraka iwezekanavya Mashariki ya Kati hata kama safari nyingi za ndege kutoka eneo hilo zimesitishwa au kuahirishwa.

Serikali ya Marekani imekuwa ikihangaika kutafuta ndege za kukodi kwa raia wa Marekani katika Umoja wa Falme za Kiarabu, Saudi Arabia na Jordan, na kutaka kuwasaidia watu waliokwama kwingine kukata tikiti za ndege za kibiashara.

Afisa wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani alisema tangu tarehe 28 Februari, takriban raia 17,500 wamerejea nyumbani kutoka Mashariki ya Kati.

Taarifa ya BBC

Share This Article