Pwani Oil kudhamini shindano la Miss Earth Kenya 2024

Martin Mwanje
2 Min Read

Kampuni ya Pwani Oil kupitia sabuni yake ya kuogea ya Afrisense, imetangaza kuwa itadhamini shindano la Miss Earth Kenya 2024.

Shindano hilo litaandaliwa baada ya kambi ya mafunzo itakayoanza Julai 16 hadi Julai 19, 2024.

Jumla ya wasichana 18 wamechaguliwa kushiriki zoezi la mchujo litakalobaini mshindi wa Miss Earth Kenya 2024 na washindi wengine watatu watajinyakulia taji la Miss Air, Miss Water, na Miss Fire mtawalia na fursa ya kufuata uongozi katika kukuza vipengele husika chini ya taji lao.

Kampuni hiyo itafadhili hafla hiyo kwa kutoa zawadi ya pesa taslimu, fursa za ubalozi, mafunzo ya miezi mitatu na ushiriki katika miradi endelevu kwa washindi.

Mshindi atavishwa taji katika hafla ya matembezi ya urembo Julai 20, 2024 katika hoteli moja jijini Nairobi.

Afrisense inalingana ipasavyo na wasifu wa shindano la Miss Earth Kenya kutokana na uundaji wake unaojumuisha viambato vya asili kama vile Kalahari Melon Seed Oil na Mafura Butter, ambavyo vimeundwa kwa njia ya kipekee kuleta asili ya urembo kwa ngozi ya Kiafrika.

Awamu ya Miss Earth Kenya 2024 iko chini ya mada “Maji ni uhai” na inakusudia kutafuta fursa za kuhifadhi maji, rasilimali muhimu ambayo mara kwa mara imekumbwa na matishio ya uchafuzi, usimamizi mbovu na hivyo kiwango chake kupungua.

Shindano la kitaifa la kila mwaka huanza na kambi ya mafunzo ambayo huwakutanisha wahitimu waliochaguliwa kwa ushirikiano na wataalamu wa uendelevu, washauri na majaji. Pia inatoa fursa kwa washiriki kujifunza kutoka kwa mabingwa wa uendelevu, ili kuongeza uwezo wao wa kuimarisha msimamo wao kama viongozi endelevu.

Beverly Jalango, mshikilizi wa Miss Earth Kenya, aliwashukuru wafadhili kama Pwani Oil kwa jukumu lao muhimu katika kutoa fursa kwa washiriki na kuitangaza Kenya katika jukwaa la kimataifa.

Ufadhili wa Pwani Oil wa Miss Earth Kenya unathibitisha kujitolea kwake kwa uendelevu wa mazingira na kusisitiza umuhimu wa ushirikiano wa makampuni katika kuleta mabadiliko chanya.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *