Rais wa Urusi Vladimir Putin leo Alhamisi ameuambia mkutano wa viongozi wakuu wa BRICS kwamba Mashariki ya Kati inakaribia kuingia katika vita kamili.
“Hatua ya kijeshi iliyoanza mwaka mmoja uliopita eneo la Gaza kwa sasa imeenea hadi nchini Lebanon. Nchi zingine katika eneo hilo pia zimeathiriwa,” Putin aliuambia mkutano huo unaofanyika katika mji wa Kazan na kuhudhuriwa na viongozi kadhaa wa dunia.
“Kiwango cha uhasama kati ya Israel na Iran kimeongezeka mno. Hii yote ni sawia na mtungo wa mwitikio na unaiweka Mashariki ya Kati yote katika hali ya kukaribia kuingia katika vita kamili,” amesema Putin.
Vurugu Mashariki ya Kati haitaisha hadi pale litakapobuniwa taifa huru la Palestina, aliongeza Putin wakati akihutubia mkutano huo ambao ulihudhuriwa na kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas.
“Takwa kuu la kurejesha amani na uthabiti katika maeneo ya Palestina linasitisha suluhu ya mataifa mawili iliyoidhinishwa na Baraza la Usalama na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa,” aliongeza Rais huyo wa Urusi.
Alisema hii itakuwa “kusahihisha madhila ya kihistoria kuelekea watu wa Palestina”.
“Hadi suala hili lisuluhishwe, haitawezekana kuvunja mduara usiomalizika wa vurugu.”