Putin akutana na kiongozi wa usalama wa Iran mjini Moscow

Huku hayo yakijiri Rais Donald Trump wa Marekani ameonya kuwa ataiangamiza Iran, hali itakayochukua takriban miaka 25 kuijenga upya.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais wa Urusi Vladimir Putin jana Alhamisi alikutana na kiongozi wa usalama wa Iran Mohsen Rezaei mjini Moscow, kujadili hali ya usalama katika kanda hiyo huku juhudi za kidiplomasia zikiendelea kukomesha vita vya Marekani na Israel nchini Iran.

Rezaei pia aliwasilisha ujumbe wa kiongozi wa kidini nchini Iran, Mojtaba Khamenei kwa Putin.

Mkutano wa Rezaei na Putni unajiri huku Qatar ikiongoeza juhudi za kidiplomasia za kumaliza vita nchini Iran, wakati hofu ikitanda kuhusu uwezekano wa Marekani kuanzisha mashambulizi mapya baada ya kumaliza uchaguzi wa katikati ya muhula.

Rezaei aliongeza kuwa Tehran haitafanya mazungumzo yoyote na Marekani kuhusu kumaliza vita au kufungua Mlango Bahari wa Hormuz hadi Washington itimize matwakwa yake saba.

Huku hayo yakijiri, Rais Donald Trump wa Marekani ameonya kuwa ataiangamiza Iran, hali itakayochukua takriban miaka 25 kuijenga upya.

Share This Article