Miamba wa Ufaransa Paris Saint-Germain wamekamilisha usajili wa kiungo chipukizi wa Brazil Gabriel Moscardo, kutoka klabu ya Corinthians.
Moscardo ametioa saini mkataba na PSG hadi Januari mwaka 2028 lakini watasalia kwa mkopo Corinthians hadi mwisho wa msimu huu.
Kinda huyo alkye na umri wa miaka 18 tayari ameichezea Corinthians mechi 25 tangu ajiunge na kikosi cha kwanza mwaka uliopita.