PSG wajiburuza hadi mchujo wa Ligi ya Mabingwa huku Newcastle wakiondokea

Dismas Otuke
1 Min Read

Klabu ya Paris St-Germain iliponea chupuchupu na kutinga raundi ya 16 bora ya kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya kulazimisha sare ya bao 1 kwa moja katika mchuano wa miwsho wa kundi F Jumatano usiku dhidi ya Borusia Dormund.

Dortmund waliongoza kupitia kwa bao Karim Adeyemi kabla ya Zaire-Emery kusawazishia PSG.

Limbukeni Newcastle United walibanduliwa baada ya kushindwa nyumbani mabao 2 kwa moja na AC Milan.

Katika matokeo mengine Barcelona walipigwa magoli 3-1 nchini Ubelgiji na klabu ya Antwerp huku Celtic ikisajili ushindi wa 2-1 dhidi ya Feyernood .

Share This Article