PSG waikwatua Sociadad na kunusia robo fainali ya ligi ya mabingwa ulaya

Dismas Otuke
1 Min Read

Miamba wa Ufaranza PSG waliwazaba Real Sociedad mabao mawili kwa nunge kupitia mshambulizi matata wa Ufaranza Kyalin Mbappe na Bradley Barcelona namo dakika ya 58 na 70 mtawalia uwanjani Parc des Princes katika mechi za raundi ya 16 bora .

Nao mabingwa mara sita wa taji hiyo Bayern Munich wa ujerumani walilazwa kwa bao moja kwa bila ugani Stadio Olimpico na wenyeji Lazio ya Italia kupitia mkwaju wa penati iliyofungwa na Ciro Immobile dakika ya 69,baada ya Dayot Upamecano kumchezea visivyo Gustavo Isaken kwenye kijisanduku na kuonyeshwa kadi nyekundu.

Mechi nyingine za awamu hiyo zitachezwa juma lijalo ,mabingwa mara tano Barcelona watakaposafiri nchini Italia ugani Diego Armando Maradon kuzichapa na Napoli.

Kivumbi kingine nchini humo baina ya washindi mara tatu na walio ibuka wa pili msimu uliopita kwa kulazwa na Mnchester City kwa bao moja kwenye fainali Intermillan watakapowakaribisha Atletico Madrid kule San Siro.

Wakati huohuo washindi mara mbili FC Porto watakabana koo na wana bunduki Arsenal, nchini Ureno nao Dortmund wajaribu kuwafuta machozi wajerumani ugani Philips nchini uholanzi dhidi ya PSV.

Share This Article