Profesa Jay achapisha picha kuonyesha yuko salama

Marion Bosire
1 Min Read
Profesa Jay

Mwanamuziki wa muda mrefu nchini Tanzania Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay alilazimika kuchapisha picha kwenye akaunti yake ya Instagram kudhibitisha kwamba yuko salama.

Chini ya picha hiyo Jay aliandika,”Asante sana Mungu kwa Zawadi ya uzima na kunilinda siku zote za maisha yangu, nipo kamiligado tayari kwa mapambano.”

Hatua hiyo inafuatia uvumi uliosambaa mitandaoni kwamba Jay ambaye pia ni mwanasiasa ameaga dunia. Vyonbo vya habari nchini humo vilichukua hatua za haraka kukomesha uvumi huo kabla ya Jay kuchapisha picha.

Tangu alipougua, Jay hajazindua kazi zozote za muziki na inasubiriwa kuona iwapo atarejelea kazi yake ya kwanza ambayo ni muziki.

Jay aliugua ugonjwa wa figo kwa muda mrefu ambapo alilazwa hospitalini kwa takribani siku 127, mwaka 2022. Baada ya hapo alianzisha wakfu kwa lengo la kusaidia wagonjwa wa figo, ambapo aliuzindua rasmi Disemba mwaka 2023.

Wasanii wengi wa Tanzania walitumia fursa ya kuchapishwa kwa picha hiyo kwenye akaunti ya Profesa Jay kumwonyesha mapenzi. Lady Jaydee alimwandikia “Kaka yanyu!”, Roma Zimbabwe akaandika, “Kila mara Yehova ni mwaminifu.” huku Zuchu akimwandikia, “Kaka Mkuu”.

Share This Article