Mawaziri wanne katika Baraza la Mawaziri lililovunjwa inaonekana wametemwa.
Hii ni baada ya nyadhifa zao kukabidhiwa watu wengine na wao kutoteuliwa katika wadhifa wowote ule.
Wao ni pamoja na aliyekuwa Waziri wa Utumishi Umma Moses Kuria. Wadhifa huo sasa umekabidhiwa aliyekuwa Mwanasheria Mkuu Justin Muturi.
Aisha Jumwa pia amepoteza wadhifa wake baada ya kuteuliwa kwa Stella Soi Lang’at kuwa Waziri mpya wa Jinsia.
Kwa upande mwingine, kuteuliwa kwa Wycliffe Oparanya kuwa Waziri mpya wa Vyama vya Ushirika kuna maana kuwa Simon Chelugui amepoteza wadhifa huo.
Mwingine aliyepoteza wadhifa wake ni Prof. Njuguna Ndung’u baada ya mbunge mteule John Mbadi kuteuliwa kuwa Waziri mpya wa Fedha.
Aliyekuwa Waziri wa Michezo Ababu Namwamba pia amepoteza wadhifa huo ambao sasa umekabidhiwa Kipchumba Murkomen.