Maafisa watano wa polisi na walimu wanne walijeruhiwa katika ajali ya barabarani jana Alhamisi jioni kwenye barabara ya Banisa-Guba, kaunti ya Mandera.
Ajali hiyo ilitokea baada ya gari la polisi kugonga mashimo mawili barabarani eneo la Armano, na kusababisha kupasuka kwa magurudumu mawili.
Waliojeruhiwa walikuwa polisi watano kutoka kituo cha Choroqo Border na walimu wa shule za msingi za Choroqo, Qotqot na Guba.