Polisi wanasa mihadarati Homabay, washukiwa watoroka

Tom Mathinji
1 Min Read
Maafisa wa DCI wanasa mihadarati Homa Bay.

Maafisa wa polisi kutoka kituo cha polisi cha Rodi kaunti ya  Homabay, wanawatafuta walanguzi wa mihadarati waliotoroka na kuacha nyuma magunia 8 ha bangi ndani ya gari.

Baada ya kupashwa habari na wananchi kuhusu gari la kutiliwa shaka lililokuwa limeegeshwa katika eneo moja la makazi, maafisa hao walifanya operesheni lakini washukiwa watatu walitoroka eneo hilo kwa kuruka ua.

Baada ya maafisa hao kupekua eneo hilo, walipata magunia 8 ya bangi ndani ya nyumba hiyo na pia ndani ya gari.

Mihadarati hiyo ilipelekwa katika kituo cha polisi cha Homa Bay, huku msako dhidi ya washukiwa hao ukiendelea.

Maafisa hao walitoa wito kwa wananchi kutoa habari zinazoweza kusababisha kukamatwa kwa washukiwa hao.

TAGGED:
Share This Article