Polisi wanasa magunia mawili ya bangi Vihiga

Dismas Otuke
0 Min Read

Maafisa wa polisi katika kaunti ya Vihiga wamenasa magunia mawili ya mihadarati inayoshukiwa kuwa bangi.

Polisi hao kutoka kituo cha Cheptulu kaunti ya Vihiga walisimamisha gari la abiria katika eneo la Sigongo ,kwenye barabara ya Chavakali–Kapsabet na makasha 14 yanayokisiwa kuwa na bangi.

Makasha hayo yalikuwa yamepakiwa ndani ya magunia mawili.

Share This Article