Maafisa wa polisi walimuua kwa kumpiga risasi mshukiwa mmoja wa ujambazi huku wawili wakitiwa nguvuni katika kaunti ya Kiambu.
Kulingana na maafisa wa polisi wa upelelezi wa jinai DCI, washukiwa watatu walimvamia mfanyabiashara mmoja alipokuwa akienda nyumbani na kumpora fedha alizokuwa amekusanya mchana mzima.
Kupitia mtandao wa X idara ya DCI ilisema maafisa wake baada ya kupashwa habari, walichukua hatua za haraka na kuwafumania majambazi hao wakiwa ndani ya mfanyabiashara huyo.
Kwa mujibu wa polisi waliamriwa kujisalimisha, lakini mmoja wao akachomoa bastola na kusababisha ufyetulianaji wa risasi. Majambazi wawili walifanikiwa kutoroka.
Polisi walipata bastola moja na risasi mbili, huku msako dhidi ya waliotoroka ukianzishwa.
Aidha baada ya msako zaidi, maafisa hao waliwakamata washirika wa majambazi hao ambao ni Elijah Mwangi Muthoni mwenye umri wa miaka 45 na David Mitamo mwenye umri wa miaka 21.