Polisi wakana kuhusika kwa utekaji nyara wa vijana wanne waliopatikana leo

Dismas Otuke
1 Min Read
Douglas Kanja - Inspekta Mkuu wa Polisi

Idara ya Kitaifa ya Polisi imekanusha kuhusika katika utekaji nyara wa vijana wanne walioachiliwa huru mapema leo Jumatatu. 

Hii ni baada ya vijana hao kutoweka katika hali ya kutatanisha mwezi jana huku polisi wakinyoshewa kidole cha lawama kwa kuwateka nyara.

Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari,  Inspekta Mkuu wa Polisi Douglas Kanja amesema Bernard Kavuli Musyimi aliyejisalimisha kwenye kituo cha polisi cha Moi’s Bridge anawasaidia maafisa wa polisi katika uchunguzi.

Ameongeza kuwa polisi pia watatafuta taarifa kutoka kwa vijana wengine waliopatikana leo ambao ni Billy Mwangi, Peter Muteti na Rony Kiplagat ili kusaidia katika uchunguzi juu ya utekaji wao.

Polisi wamewataka wananchi kutoa taarifa zozote walizo nazo kuhusu utekaji nyara huo kupitia kwa nambari za simu bila malipo 999, 911 na 112 ili kusaidia kwa uchunguzi.

Kwenye taarifa iliyotumwa kwa niaba yake na msemaji wa polisi Dkt. Resila Onyango, Kanja amesema wanaendelea na uchunguzi kuhusu visa vingine vyote vya utekaji nyara kote nchini ili kubaini chanzo na wahusika wakuu.

 

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *