Maafisa wa polisi nchini Ufaransa wameanza kufunga barabara za jiji kuu la Paris, kwa matayrisho ya sherehe za kufungua makala ya 33 ya michezo ya Olimpiki itakayoandaliwa katika mto Siene Julai 26.
Sherehe za ufunguzi zitaandaliwa kwenye upana wa kilomita sita katika mto Siene huku barabara zote za kuelekea mto huo zikifungwa kwa sasa.
Itakuwa mara ya kwanza kwa sherehe za kufungua michezo ya Olimpiki kuandaliwa nje ya uwanja .
Polisi wapatao 45,000 wakisaidiwa na watoa usalama wa kibinafsi na polisi wa kawaida watashika doria Julai 26, wakati wa sherehe za ufunguzi.
Kndi la kwanza la wanamichezo linatarajiwa kuwasili siku ya Alhamisi katika kijiji cha wanamichezo tayari kwa Olimpiki.
Wanamichezo watakaowasili Alhamisi ni kutoka mataifa ya Uingereza,Marekani, New Zealand, Brazil na Uswizi.
Kijiji hicho kina uwezo wa kuselehi watu 14,500 wakiwemo wanamichezo 9,000.