Maafisa wa upelelezi wameanzisha uchunguzi kuhusu mauji ya mwanafunzi mmoja wa kike wa umri wa miaka 19 aliyepatikana ameuawa mjini Thika.
Mwili wa marehemu kwa jina Faith Musembi aliyekuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika chuo kikuu cha Mt Kenya bewa kuu la Thika, ulipatikana chumbani mwake mtaani Pilot Estate.
Babake kwa jina Boniface Musembi ndiye aliyepata mwili wa marehemu bintinye katika chumba alichopangisha mjini Thika na kuongeza kuwa walipakea simu kutoka kwa mtu asiyejulikana aliyekuwa amemteka nyara na alipwe kombozi ya shilingi 20,000, ndiposa amwachilie.
Kulingana na babake,mtekaji nyara huyo alitumia simu ya bintiye kumpigia na mamake akatuma hela hizo huku akiripoti katika kituo cha polisi ambao anadai hawakuchukua hatua zozote.
Yamkini Faith aliuawa Jumatano iliyopita .
Mwili wa marehemu ulipatikana kitandani ukiwa unavuja damu .