Polisi waanzisha msako wa mshukiwa wa mauaji ya mhasibu wa Hospitali ya Nairobi

Dismas Otuke
1 Min Read

Idara ya upelelezi wa kesi za jinai imetoa taarifa kwa umma kuhusu yeyote aliye na habari kuhusu mwanamke ambaye ni mshukiwa mkuu katika muaji ya mhasibu wa Hospitali Nairobi .

Kupitia kwa mtandao wake wa X DCI imetoa picha zilizonaswa na Camera za CCT zikionyesha mwanamke huyo akitoroka kutoka kwa boma la marehemu na akiruka ua.


Mwili wa Eric Maigo ulipatikana na majeraha 25 ya kisu nyumbani kwake mtaani Woodley.

Marehemu alipatikana ameuawa mapem Ijumaa Septemba 15 .

DCI wameomba umma kuwasilisha ripoti zitakazopelekea kukamatwa kwa mshukiwa huyo mkuu .

Share This Article