Polisi wameanzisha uchunguzi kubaini chanzo cha moto ulioteketeza karakana moja ya magari katika kaunti Kiambu jana Jumatano.
Magari manane ya kifahari yaliteketea wakati wa kisa hicho.
Magari hayo yalikuwa kwenye karakana ya kukarabati magari ya Jua Kali, wakati moto ulipozuka na kuharibu mali ya thamani ya mamilioni ya pesa.
Hata hivyo, moto huo ulizimwa na wazimamoto wa serikai ya kaunti ya Kiambu.
Vyanzo vya awali vya polisi vinaashiria kuwa moto huo ulioanzia kenye karakakana hiyo kabla ya kuenea, ulisababishwa na kulipuka kwa mtungi wa gesi.
Aina ya magari yaliyoteketea ni pamoja na Toyota NZE, magari matano aina ya Nissan Matatu, gari moja la Toyota 71, na lingine moja la Toyota Prado.