Polisi wa kukabiliana na ghasia kwa siku ya tatu wamefunga barabara ya kuelekea Ikulu ya Nairobi, kwa waendeshaji magari na wanaotembea kwa miguu .
Hatua hiyo imechukuliwa kukabiliana na waandamanaji wanaopinga mswada wa fedha wa mwaka 2024 waliotishia kuvamia ikulu.
Haya yanajiri huku zaidi ya vijana 500 wakiandamana Jumapili na kukutana katika bustani ya Jivanjee jijini Nairobi, kuomboleza wenzao waliouawa kwenye maandamano na maafisa wa polisi.
Kulingana na takwimu za makundi ya wanaharakati watu 23 wameuawa tangu kuanza kwa maandamano hayo, huku wengine wakiwa hawajulikani waliko baada ya kutekwa nyara.