Polisi wa Kenya waendelea kushika doria Haiti

Dismas Otuke
1 Min Read

Polisi wa Kenya waliendelea kushika doria katika mji mkuu wa Haiti Port Au Prince, kwa wiki ya pili tangu kuwasili nchini humo  baada ya kutumwa na serikali ya Kenya.

Polisi hao ni mojawapo wa mikakati na ombi la Umoja wa mataifa na Marekani kama njia ya kurejesha utulivu nchini humo, baada ya magenge ya majambazi kusababisha vurumai.

Mji huo mkuu kwa sasa unathibitiwa kwa asilimia 80 na magenge ya majangili, huku zaidi ya watu 580,000 wakifurushwa makwao.

Kundi la kwanza la polisi 400 liliwasili nchini Haiti Juni 25 huku Waziri Mkuu wa taifa hilo Garry Conille, akikiriri kuwa takriban raia milioni 12 wametekwa nyara na majangili 12,000.

Polisi wa Kenya wanatarajiwa kupigwa jeki na wengine 1,500 kutoka Bahamas, Bangladesh, Barbados, Benin, Chad na Jamaica, ambao watafikisha idadi ya maafisa wa usalama 2,500.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *