Maafisa wa polisi eneo la Eldama Ravine, kauti ya Baringo, wanachunguza mauaji ya mwanamke mwenye umri wa miaka 32, anayeaminika kuuawa na aliyekuwa mume wake.
Kulingana na idara ya upelelezi wa makosa ya jinai, mauaji hayo yanaaminika yalitekelezwa na mume wake wa zamani, aada ya kugundua kwamba mwanamamke huyo sasa ana mpenzi mwingine.
Kulingana na majirani, mwanamke huyo alionekana akielekea nyumbani kwa mpenzi wake wa sasa Jumatatu saa mbili usiku, kabla ya mwili wake kupatikana saa tatu usiku, ukiwa na majeraha ya kukatwa kichwani.
Maafisa wa upelelezi wa DCI kutoka kituo cha polisi cha Koibatek, wameanzisha uchunguzi, huku mumwe wake wa zamani Alex Kimeli Ng’elel ambaye ndiye mshukiwa mkuu wa mauaji hayo aliye mafichoni, akisakwa na polisi.