Police FC wana mtihani mgumu dhidi ya miamba Zamalek Jumamosi

Dismas Otuke
1 Min Read

Klabu ya Police FC ya Kenya  itakabiliwa na kibarua kigumu itakapochuana na mabingwa watetezi Zamalek ya Misri Jumamosi, kuanzia saa tisa uwanjani Nyayo katika mkumbo wa kwanza wa mchujo wa pili kuwania kombe la Shirikisho.

Itakuwa mara ya kwanza kwa timu hizo mbili kukutana katika mashindano ya Afrika.

Zamalek walinyakua kombe hilo mwaka jana baada ya kuishinda RS Berkane kwa bao la ugenini baada ya fainali hiyo kumalizia sare ya 2-2, na watakuwa wanacheza kwa mara ya kwanza msimu huu baada ya kuepushwa mchujo.

Zamalek wakifanya mazoezi Ijumaa uwanjani Nyayo

Polisi nao walitinga mchujo wa pili baada ya kuibandua Ethiopia Coffee  bao 1-0 katika mchujo wa kwanza.

Mechi ya marudio itasakatwa wikedni ijayo nchini Misri huku mshindi wa jumla akifuzu kwa hatua ya makundi.

 

Share This Article