Police FC walazwa chali nyumbani na Mwarabu

Dismas Otuke
1 Min Read

Matumaini ya klabu ya Kenya Police kufuzu kwa hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho Afrika yamedidimia, baada ya kulazwa na mabingwa watetezi Zamalek SC ya Misri, karika mkondo wa kwanza wa mchujo wa pili.

Mechi hiyo imesakatwa Jumamosi katika uwanja wa Taifa wa Nyayo.

Bao pekee na la ushindi kwa wageni lilitiwa kimiani na kiungo Abdallah Sayed, kunako dakika ya kwanza ya mazidadi kipindi cha kwanza.

Pambao la marudio litaandaliwa wiki ijayo huku Police, wahitaji ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya miamba hao, ili kutinga hatua ya makundi.

Share This Article