Mabingwa watetexi Gor Mahia wameambulia kichapo cha tatu katika ligi kuu ya FKF baada ya kulazwa bao moja kwa bila na Police FC katika uwanja wa Sportpesa mjini Murang’a leo.
Alvin Mangeni aliwafungia maafande bao la pekee kunako dakika ya 63,akiunganisha mkwaju wa kona wa Daniel Sakari, na kuwapokeza Gor kichapo cha tatu msimu huu.
Katika pambano jingine Mara Sugar FC imewaadhibu Kariobangi Sharks goli moja bila jibu, nao FC Talanta na Nairobi City Stars wakitoka sare ya bao moja .
Kakamega Homeboyz na Ulinzi Stars pia waligawana alama moja baada ya kuambulia sare ya goli moja.