Vidosho wa Kenya Pipeline wamefuzu kwa fainali ya mashindano ya Afrika Mashariki na kati yanayoendelea mjini Kigali ,Rwanda baada ya kuwashinda National Police ya Rwanda seto 3-1 katika mechi ya mwisho ya makundi siku ya Ijumaa.
KPA wameshinda mchuano huo alama 25-16,23-25,25-14 na 25-23 na watachuana na Rwanda Patriotic Army katika mechi ya mwisho ya mzunguko, kabla ya kucheza fainali Jumapili hii.
KPA walifungua mashindanoi hayo kwa ushindi wa seti 3-1 dhidi ya Kampala City Council Authority kabla ya kuwalemea Rwanda Revenue Authority.