Mwanamuziki nguli wa nyimbo za injili Dkt. Pete Odera, anasababu ya kutabasamu baada ya kuongeza idadi ya tuzo, aliposhangaza ulimwengu kwa kuibuka mshindi katika makala ya 39 ya tuzo za Stellar zilizoandaliwa Las Vegas, Nevada.
Odera aliyekuwa amejawa na furaha si haba, aliwashukuru wasikilizaji wake kwa kuiweka Kenya kwenye ramani ya ulimwengu katika nyimbo za injili na kwa kuunga mkono Afrika kupitia nyimbo hizo.
GODRADIO1, jukwaa ambalo hutumiwa kupeperusha kipindi Good Morning Africa, kilipiku vipindi vingine vingi kutoka Marekani na ulimwengu kwa jumla na kuibuka mshindi wa tuzo ya stesheni ya mwaka ya intaneti.
Dkt. Pete Odera na wenzake Walter KO, Robert Earl Dean na mkurugenzi wa vipindi Michelle Thompson, walipokea tuzo hiyo wakati wa sherehe iliyoandaliwa katika hoteli moja ya kifahari Julai 19, 2024.
Tye Tribbett alishinda tuzo ya wimbo bora wa mwaka, huku Ricky Dillard ikishinda tuzo ya kwaya ya mwaka.