Bingwa wa London Marathon na mshikilizi wa zamani wa rekodi ya dunia ya nusu marathon Peres Jepchirchir wa Kenya, ametoa ithibati kushiriki makala ya mwaka huu ya mbio za Vedanta Delhi Half Marathon.
Mbio hzo zitaandaliwa Oktoba 20 nchini India huku Jepchirchir ambaye ni bingwa wa Olimpiki wa marathon mwaka 2020, akiwania ushindi baada ya kutwaa ubingwa wa dunia wa nusu marathon mara tatu.
Makala ya mwaka huu yatakuwa na kitita cha zawadi ya pesa ambazo ni jumla ya shiloingu milioni 32.5 za Kenya, huku washindi wa mbio za wanaume na wanawake wakitia mkobani shilingi milioni 3.2 kila mmoja.
Pia watakaovunja rekodi watatuzwa shilingi milioni 1.5
Jepchirichir atawinda ushindi mwingine nchini India, baada ya kushinda mbio za TCS World 10K Bengaluru mwaka 2016.