Paul Bitok ajiuzulu kutoka Malkia Strikers

Dismas Otuke
1 Min Read

Naibu kocha wa timu ya taifa ya Voliboli ya Kenya kwa akina dada maarufu kama Malkia Strikers ,Paul Bitok amejiuzuku kutoka wadhfa huo.

Bitok ambaye alikuwa atimize miaka minane akiwa na Malkia Strikers,amesema ameafikia uamuzi huo baada ya kushauriana kwa kina na familia yake.

Kocha huyo alikuwa aandanane na timu ya Kenya kwa michezo ya Olimpiki jijini Paris Ufaransa mwaka huu.

Kujiuzulu kwake kunaaminika kutokana na shutuma kali kutoka kwa umma baada ya kocha huyo kuteuliwa mmoja wa maafisa watakaelekea Ufaransa, kwa michezo ya Olimpiki pamoja na Kinara wa shirikisho la Voliboli Charles Nyaberi.

Share This Article