Pascal Tokodi azungumzia talaka

Anasema talaka yao ilistahili kuwa ya kimya kimya lakini mambo yalivujishwa mitandaoni.

Marion Bosire
2 Min Read
Pascal Tokodi

Mwigizaji Pascal Tokodi amezungumzia talaka yake na Grace Ekirapa, akisema ingawa ndoa yake ilipaswa kuwa na faragha, uhusiano wao uliangaziwa baada ya picha za harusi yao kuvuja kwenye mitandao ya kijamii Septemba 2020.

Anaongeza kwamba hata baada yake na Ekirapa kutengana kimya kimya, hilo pia lilisambazwa.

Tokodi anasema hatua ya vyombo vya habari kuangazia talaka yake ilimshangaza na ni uvamizi wa faragha huku akihisi kwamba watu wanapaswa kuheshimu faragha ya kila mmoja na kujikita katika maisha yao wenyewe.

Mwigizaji huyo nguli anafafanua kuwa hajapata nafasi ya kuzungumzia kutengana kwake na Ekirapa hadharani kwenye mitandao ya kijamii kwa sababu hatumii akaunti zake kuangazia mambo ya kibinafsi.

“Mitandao ya kijamii sio mahali pa kutangaza mambo yako. Watu wengi mitandaoni hatujuani.” alisema Tokodi huku akipendekeza kuzungumza na mtaalamu au mtu wa kuaminika anayeweza kusaidia kuelewa mambo nje ya macho ya umma.

Kuhusu kulea mtoto wao pamoja, mwigizaji anathibitisha kwamba ni safari rahisi na mke wake wa zamani.

“Kulea mtoto na Grace ni jambo la ajabu. Grace ni mwanamke mzuri, na akiwa mama wa mtoto wangu, nina uhakika binti yangu atapata msingi bora anaostahili,” anasema mwigizaji huyo.

Wawili hao walitengana kimya kimya mwanzo wa mwaka 2024 baada ya ndoa ya miaka mitatu.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *