Beki wa timu ya taifa ya soka ya Kenya, Harambee Stars, Eric Marcelo Ouma, ameachwa nje ya kikosi cha Harambee Stars kwa mechi mbili za mwezi ujao kufuzu kwa Kombe la Dunia kwa sababu ya jeraha.
Ouma kupitia kwa mitandao yake ya kijamii amesema alipata jeraha la mguu akiwa mazoezini na hawataweza kuchezea klabu yake wala timu ya taifa.
Harambee Stars itawaalika Gambia Septemba 5, kabla ya kuchuana na Ushelisheli ,siku nne baadaye, mechi zote zikipigwa uwanjani Kasarani.
Mlinzi huyo aliye na umri wa miaka 28, anachezea klabu ya Raków Częstochowa nchini Poland.