Otto Addo ameteuliwa tena kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ghana Balck Stars na chama cha soka nchini humo GFA.
Addo aliye na umri wa miaka 47 amerejeshwa usukani miezi 15, baada ya kuingoza Black Stars katika kipute cha Kombe la Dunia nchini Qatar.
Addo anatwaa mikoba ya ukufunzi kutoka kwa
Chris Hughton, aliyepigwa kalamu kufuatia matokeo duni ya Black Stars katika fainali za AFCON nchini Ivory Coast.
Kulingana na GFA Addo amepewa kondrati ya miezi 34, lakini ana uwezo wa kuingeza kwa miaka miwili zaidi .
Kocha huyo kwasasa ni mojawapo wa kikosi cha ukufunzi katika klabu ya Borussia Dortmund atakapogura mwezi Mei mwaka huu, ili kuanza majukumu yake mapya.