Mwanamuziki wa Kenya Otile Brown ameibuka kidedea kwa idadi jumla ya mitazamo ya kazi zake za sanaa kwenye jukwaa la mitandaoni la YouTube.
Kulingana na takwimu kazi za msanii huyo au ukipenda video zimetizamwa mara milioni 545, idadi ambayo ndiyo ya juu zaidi kati ya wanamuziki wa taifa hili.
Anafuatiwa na kundi la Sauti Sol milioni 448, huku Willy Pozee au Willy Paula akiwa nambari 3 na mitazamo milioni 400.
Kwaya ya nyimbo za injili ya Msanii Music Group inafuata kwa mitanzamo milioni 385, Nambari 5 ni Bahati akiwa na mitazamo milioni 350 akifuatiwa na mkewe Diana B aliye na jumla ya mitazamo milioni 349,
Prince Indah, Gurdian Angel, Nyashinski na marehemu John De’Matthew wanakamilisha orodha ya 10 bora kwenye YouTube nchini Kenya kwa mitazamo milioni 297, 272, 232 na 225 mtawalia.